Alipa milioni 5 kukwepa kifungo cha mwaka mmoja jela [NimasikaForum]
Na Karama Kenyunko
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu John Chuwa mkazi wa Barakuda jijini Dar es Salaam, kulipa faini ya sh. milioni 5 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada kupatikana na hatia kwa kosa la kuchapisha maudhui katika mtandao wa Youtube bila kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Hukumu hiyo imesomwa leo Juni 7, 2019 katika na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde baada ya mshtakiwa kukiri makosa yake hayo.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kasonde amesema, kwa kuwa mshtakiwa amekiri makosa yake yeye mwenyewe na kwamba hajaisumbua mahakama anatiwa hatiani kwa kosa hilo. Ambapo kabla ya kutoa adhabu, alimtaka mshtakiwa kujitetea, nae akaiomba mahakama isimpe adhabu kali kwani mama yake mzazi na wadogo zake wawili wanamtegemea hivyo akipewa adhabu ya kwenda jela watapata tabu.
Mapema, wakili wa Serikali Elizabeth Mkunde, alimsomea mshtakiwa maelezo ya awali na kudai mwaka 2018 mshtakiwa alifungua mtandao wa YouTube kwa kutumia barua pepe ya jalifilmstz@gmail.com ambamo alikuwa akitoa matangazo ya filamu za kitanzania kupitia simu yake ya mkononi aina ya Huawei Y9 huku akijua hana kibali kutoka TCRA.
Amedai, mshtakiwa alipokamatwa alikutwa na simu mbili za mkononi Huawei na Nokia.
Baada ya kusomwa kwa maelezo hayo, wakili huyo wa Serikali, Mkunde alidai, kwa sababu mshtakiwa amekiri makosa yake yeye mwenyewe basi anaiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hizo.
Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa katika terehe tofauti kati ya 2018 na Aprili 2019 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alichapisha maudhui kupitia mtandao wa Youtube uitwao John Film Entertainment bila kuwa na kibali kutoka TCRA.
Mshitakiwa huyo aliposomewa shtaka lake Juno 4, 2019 alikiri kutenda kosa hilo na alichiwa kwa dhamana hadi leo alipohukumiwa adhabu hiyo ambapo amefanikiwa kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.

No comments