DIWANI MSOPHE ATOA MSAADA WA VYAKULA,SABUNI NA MADAFTARI KWA MAKUNDI YENYE UHITAJI KIPUNGUNI [MamboPulse]
Na Saidi Mwishehe,Globu ya jamii
DIWANI wa Kata ya Kipunguni iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam Mohammed Msophe ameamua kutoa msaada wa vyakula na sabuni kwa wajane, walemavu ma watoto yatima.
Mbali na kutoa msaada wa vyakula na ,sabuni pia ametoa msaada wa madaftari na kalamu kwa wanafunzi waliopo ndani ya Kata hiyo wanaosoma shule za msingi na sekondari ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha elimu na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya tano chini ya uongozi mhari wa Rais Dk.John Magufuli ambayo imeamua elimu ya msingi na sekondari iwe bure.
Akizungumza leo wakati wa ugawaji msaada huo kwa makundi hayo Diwani Msofe amesema msaada huo umetoka kwa marafiki zake waliotaka kusaidiwa kwa makundi hayo,hivyo yeye amewezesha msaada huo kufika kwa walengwa walioko kwenye kata yake.
"Marafiki zangu ndio walioamua kutoa msaada huu,nami jukumu langu ni kuhakikisha makundi ambayo yanatakiwa kupatiwa msaada huu.Asilimia 95 ya waliopata msaada ni watu wenye walemavu,watoto yatima,wajane na wale wanatoka kwenye familia za wasiojiweza kutokana na sababu mbalimbali.
"Pia tumetoa msaada kwa kugawa madaftari,panseli na kalamu kwa wanafunzi,lengo ni kuhamasisha elimu ndani ya Kata yetu na wakati huo huo kuunga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa katika ya sekta ya elimu,kwani tunatambua Serikali ilitangaza elimu bure kwa shule za msingi na sekondari,"amesema Msophe.
Amefafanua matarajio yao ni kusaidia wananchi 3000 waliopo katika Kata hiyo huku akielezea kupitia marafiki zake wamekuwa wakisaidia jamii kwa kutoa msaada ya kijamii na kuahidi kuendelea kufanya hivyo kadri watakavyopata.
Wakati huo huo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ndani ya Kata hiyo pamoja na mafanikio ,kilio cha wananchi ni sekondari ya Kata kwani wanafunzi wanalazimika kwenda mbali mrefu,hivyo ombi lao ni kujengewa sekondari na tayari eneo limepatikana na kinachohitajika ni fidia.
Pia amesema changamoto nyingine ni kulosekana kwa kituo cha afya cha kata huku akieleza tayari msingi ulishaanza kujengwa ,hivyo Serikali inaweza kuendelea kwa kuanzia hapo."Changamoto kubwa ni kulosekana kwa kituo cha afya cha Kata,tayari tulishaanza kutafuta ufumbuzi kwa kuanza ujenzi wa msingi.Tunaomba Serikali itusaidie."
Diwani Msophe pia amesema kuna changamoto ya barabara ambapo amesema anafahamu mikakati ya Serikali katika kuboresha miundombinu ya barabara,hivyo ombi la wananchi ni kuona barabara yao inakuwepo kwenye mpango wa kuboreshwa.
Kwa upende wa wananchi wa Kata hiyo ikiwemo Mariamu Mwinyimvua na Athanas Michael wamesema wanampongeza Diwani wao kwa kujali na kuthamini makundi yenye uhitaji ambapo kupitia marafiki zake amewezesha kupatikana kwa msaada huo.
Wamesema kikubwa ambacho wanakitamaza wao sio udogo au ukubwa wa msaada ambao wameupata bali wanauona upendo,huruma na unyenyekevu wa Msophe kwa wananchi anawatumikia vila kujali hali zao.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kipunguni wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuchukua msaada wa vyakula na sabuni kutoka kwa Diwani wa kata hiyo
Diwani wa Kata ya Kipunguni Mohammed Msophe akiwaa ameshikana mkono na mmoja ya wakati wa kata hiyo baada ya kumkabidhi msaada wa McHale,maharege na sabuni.Diwani huyo leo America msaada wa vyakula ,madaftari na sabuni kwa wananchi wenye uhitaji maalum wakiwamo walemavu,wajane,yatima na wasiojiweza.
Mmoja wa wananchi wa Kata ya Kipunguni jijini Dar es Slaam akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Diwani wa kata hiyo Mohammed Msophe
Diwani wa Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam akikabidhi msaada wa madaftari na kalamu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioko ndani hiyo
Diwani wa Kipunguni Mohammed Msophe akikabidhi msaada wa vyakula na sabuni kwa moja ya wakati wa kazi wa kata hiyo wakati wa utoaji msaada wa vyakula,sabuni na madaftari
Sehemu ya wananchi wa Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam wakiwa nje ya Ofisi za Serikali ya Mtaa wakisubiri kuingia ndani kwenda kuchukua msaada wa vyakula kutoka kwa Diwani wao Mohammed Msophe
No comments