tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

eGA yakabidhi mfumo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali [NimasikaForum]

 Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Clement  Mashamba akizungumza wakati wa kupokea mfumo wa Kieletroniki kutoka Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) jijini  Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Huduma za Tehama wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Injinia Benedict Ndomba akitoa maelezo ya mfumo kwa Wakili Mkuu wa Serikali  wakati wa makabidhiano yaliiyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Ubora na Udhibiti wa Mashauri wa  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali  Evarist Mashiba akitoa maelezo watavyosimamia mfumo katika utoaji  huduma kwa wadau,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  wa Usimamizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama)  wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Injinia Benedict Ndomba akizungumza wakati wa Kukabidhi mfumi kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) umeikabidhi Mfumo wa Kieletroniki Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mfumo katika kutika kurahisisha utoaji wa taarifa kwa wadau wa utoaji haki na Maamuzi katika mashauri mbalimbali.

Akizungumza na waandishi  habari wakati wa makabidhiano hayo   Mkurugenzi wa Usimamizi wa  Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Injinia Benedict Ndomba amesema wametengeneza mfumo huo ili kukidhi mahitaji ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika kurahisisha utoaji wa huduma wa Taasisi za Serikali.

Amesema katika awamu ya kwanza imetengenezwa moduli itakayosaidia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika kutekeleza majukumu mbalimbali yanayohusiana na majalada ya mashauri na wanauwezo wa kuongeza kutokana na mahitaji ya Ofisi hiyo.

Wakili Mkuu wa Serikali  Dkt.Clement Mashamba amesema mfumo huo umetengenezwa kwa wakati na kuzingatia mahitaji yaliyoainishwa na ofisi yake kwa sasa na kuwa karibu na eGA ili kuendesha kazi kwa ufanisi.

"Mfumo huu kwetu utasaidia kuboresha usimamizi wa mashauri ikiwa ni pamoja na udhibiti ubora wa huduma zinazotolewa na ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na kuongeza kasi ya utendaji wa ofisi kwa wadau " amesema Dkt. Mashamba

Mkurugenzi wa usimamizi wa mashauri na udhibiti ubora Evarist Mashiba ameeleza kuwa mfumo huo utasaidia shughuli za upokeaji na usimamizi wa mashauri kutoka mahakamani. 

"Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilikuwa haina mfumo wa kieletroniki kukabidhiwa kwa mfumo huu utawezesha kuharakisha shughuli zote za usimamizi wa mashauri na maamuzi kwa wadau wetu.ameeleza Mashiba.

This post appeared first on Nimasika Forum
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.