HATIMAE WAISLAM WAKABIDHIWA KIWANJA CHAO CHA OMUGAKORONGO - KARAGWE . [NimasikaForum]
Anaadika Abdullatif Yunus wa Michuzi Tv - Karagwe .
Mgogoro uliofukuta takribani Miaka 30 ukihusisha Waislam wa Wilayani Karagwe Mkoani Kagera, dhidi ya wavamizi 14 waliovamia Eneo la Ardhi ya Waislam hao lililopo Omugakorongo, Kayanga Karagwe umemalizika baada ya Serikali kulikabidhi rasmi eneo hilo kwa Waislam.
Akikabidhi Eneo hilo mnamo June 7, 2019 kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka, kwanza amewashukuru wale wote waliowahi kuvamia Eneo hilo na kisha wakajiondoa kwa hiari, pili na kuwataka wale ambao wamebaki kuondoka Mara moja ili Wenye haki ya kumiliki Eneo hilo wafanye mambo yao.
Aidha Mhe. Mheluka akikabidhi Eneo hilo baada ya kulikagua na kujiridhisha, amewataka Waislam kushughulikia upimaji wa eneo lao, akiaahidi kutoa usaidizi wa jambo hilo, na pia kuwataka kuliendeleza kwa shughuli mbalimbali huku akisisitiza kuwa Serikali haipo Tayari kuona eneo kubwa kama hilo likiwa limebaki wazi bila kuliendeleza.
Itakumbukwa kuwa Eneo hilo lenye ukubwa wa Hekali 13, hapo awali Waislam walilipata kutoka Serikali ya kijiji (Abakungu), na kukabidhiwa kwa Taasisi iliyokuwa inasimamia masuala ya kiislam ya East Africa Muslim Welfare Society (EMWAS) Mwaka 1990, ambapo mnamo 1968 Taasisi hiyo ilivunjwa na Kuundwa (BAKWATA) hivyo Mali zote kikiwemo kiwanja hicho zilizokuwa wakakabidhiwa Bakwata.
Pamoja na ucheleweshwaji wa haki hiyo, tayari BAKWATA wameshinda shitaka lao katika mahakama ya Ardhi ya Kata, Wilaya, licha ya mvamizi mmoja kukata rufaa bado pia ameshindwa katika shitaka hilo.
Download


Pichani Mkuu wa Wilaya Karagwe, Mhe. Mheluka (Mwenye Suti) akiwa na waumini na Sheikh wa (W) Karagwe, wakitembelea na kukagua kiwanja cha Omugakorongo Karagwe ambacho kimekuwa na mgogoro kwa kipindi kirefu.
Pichani ni eneo ambalo miaka ya 1968 palijengwa msikiti mahala hapa, na kubomolewa na wavamizi, licha mabaki ya vipande vya tofali kusalia sehemu hii.
Sehemu ya Waumini wa Kiislam Karagwe wakiendelea kuwasikiliza Viongozi kabla ya kukabidhiwa Eneo lao.
Pichani ni Sheikh wa (W) Karagwe, Nassib Abdul, akitoa Maelezo machache kwa Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheluka, katika ni Sheikh wa (W) Kyerwa.









No comments