tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

Huawei wapigwa stop Facebook [MamboPulse]

No photo description available.

Kampuni ya Facebook imeingia rasmi katika vita vya kiuchumi baina ya Marekani na China ikizuia huduma wezeshi (APP) zake kutumika katika simu za Huawei.
Zuio hilo linalenga huduma mama ya Facebook na nyingine kutoka kwa kampuni washirika ambazo ni WhatsApp na Instagram.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Marekani mwezi Mei kuzuia kampuni za Marekani kutumia huduma za Huawei kutoka China, ikieleza ni “sababu za kiusalama”.

Hata hivyo, watu ambao tayari wamenunua simu za Huawei na wanapata huduma husika wataendelea kuzitumia isipokuwa wale wapya.

Facebook imesema pia itaendelea kusambaza huduma za kuweka mambo mapya (updates) kwa wamiliki wa sasa wa simu za Huawei.

Kampuni ya Huawei haijatoa taarifa yoyote kuhusu uamuzi huo wa Facebook.

Uamuzi huo unawahusu wateja ambao tayari walikuwa wanatumia huduma hizo na si wale wanaotaka kupakua pale wanapotaka kuanza kutumia simu mpya za Huawei.

This post appeared first on Mambo Pulse
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.