tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

IRAN YAZINDUA MFUMO WA KISASA WA MAKOMBORA [MamboPulse]



Nchi ya Iran imezindua mfumo wa kujilinda kwa makombora uliotengenezwa kikamilifu nchini humo unaoweza kulenga shabaha sita za adui kwa wakati mmoja. 

Mfumo huo wa makombora uliopewa jina la 'Khordad 15' umezinduliwa mbele ya Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami mapema leo hii. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa, mfumo wa makombora wa 'Khordad 15' una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita 120. 

Ameongeza kuwa mfumo huo wa makombora una uwezo wa kugundua maeneo ya siri na kuyasambaratisha katika umbali wa kilomita 45. 

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameeleza pia kwamba mfumo wa ulinzi wa 'Khordad 15' unatumia makombora ya 'Sayyad 3' na una uwezo wa kugundua, kusambaratisha na kutungua shabaha sita kwa wakati mmoja. 

Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunda mifumo mbalimbali ya kukabiliana na makombora na vitisho vingine vya anga kwa kuzingatia kuwepo vikosi vya kikanda katika kambi za nchi zinazoziunguka Iran. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwa ajili ya kujilinda na si tishio kwa nchi nyingine. 

Tujikumbushe kidogo kuwa pia iran ina mfumo wa 'Bavar-373' ambao unapiga kazi kama mfumo wa 's300' wa urusi. 


This post appeared first on Mambo Pulse
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.