tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

LEO KATIKA HISTORIA: Carlo Ancelotti, kocha mwenye mafanikio Ulaya [MamboPulse]



Carlo Ancelotti ni kocha wa sasa wa klabu ya Napoli. Mchezaji huyo wa zamani wa Italia alizaliwa Juni 10, 1959 katika mji mdogo wa Reggiolo kwenye jimbo la Emilio Romagna nchini Italia. 

Ancellotti alianza kucheza soka mwaka 1973 katika klabu ya vijana ya Reggiolo na baadaye klabu ya Parma. Soka la kulipwa alianza mwaka 1976 katika klabu ya Parma mwaka 1976 baada ya kupandishwa kutoka timu ya vijana. 

Ancelotti ni miongoni mwa makocha watatu ambao wametwaa taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UCL) mara tatu. Mara mbili akiwa na AC Milan na moja akiwa na Real Madrid. Pia ni miongoni mwa makocha wawili waliofika  fainali nne za Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ancelotti ametwaa taji la Kimataifa la Vilabu duniani maarufu FIFA Club World Cup mara mbili akiwa na Milan na Real Madrid. 

Aidha Ancelotti ni miongoni mwa watu saba ambao wameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa wachezaji na kama kocha. Ancelotti anachukuliwa kama  miongoni mwa makocha waliopata mafanikio makubwa wa zama zote. Enzi zake za uchezaji alicheza kama kiungo akiisaidia Parma kwenda Serie B mwaka 1979 na msimu uliofuata alitua AS Roma ambako alitwaa taji la Serie A na mataji manne ya Coppa Italia. 

Akiwa na Milan miaka ya 1980 alishinda mataji mawili ya ligi kuu na ligi ya mabingwa mara mbili. Katika timu ya taifa alicheza mechi 26 akifunga bao moja. Alishiriki kombe la dunia mara mbili; mwaka 1990 Italia ilishika nafasi ya tatu huku mwaka 1988 aliisaidia Italia kufika nusu fainali katika ya Euro. 

Akiwa kocha amezinoa Reggiana, Parma, Juventus, Milan, Chelsea, PSG, Real Madrid, Bayern Munich na ameshinda mataji katika nchi alizonoa timu hizo.


This post appeared first on Mambo Pulse
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.