Mabilionea 100 wa Magufuli walivyowaibua Zitto, Lema mitandaoni [MamboPulse]
By Exaud Mtei, Mwananchi emtei@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Si unakumbuka kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa jana Ijumaa Juni 7, 2019 Ikulu Dar es Salaam kwamba anatamani atakapomaliza muda wake wa uongozi aache mabilionea 100 nchini Tanzania.
Kiongozi mkuu huyo wa Tanzania alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini kwenye mkutano wa siku nzima uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Katika mkutano huo wafanyabiashara hao walieleza changamoto wanazokumbana nazo na kujibiwa na Rais Magufuli, mawaziri na watendaji wa taasisi za Serikali ambao pia walieleza mikakati mbalimbali iliyofanyika na inayoendelea kufanyika ili kumaliza changamoto hizo.
Kauli hiyo ya Magufuli imeonekana kuwakuna baadhi ya wanasiasa, akiwemo mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe na mwenzake wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambao walitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kueleza hisia zao kutokana na kauli hiyo ya Magufuli.
Lema alieleza kuwa hotuba ya Rais Magufuli katika mkutano huo imejaa matumaini hasa kwa kauli yake ya kuacha mabilionea 100.
“Kauli ya Rais kuwa anataka kuona Tanzania ya mabilionea100 kabla ya kumaliza muda wake wa uongozi ni kauli ya matumaini kwa nchi.”
This post appeared first on Mambo Pulse

No comments