tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

MASHINDANO YA MISS ARUSHA YAZINDULIWA RASMI [MamboPulse]

Warembo wanaopambania taji la miss Arusha wakiwa wamejipanga tayari kwa kumpokea ngeni rasmi katika Hotel ya Kibo Palace leo Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya miss Arusha kama wanavyoonekana pichani.Picha na habari na Vero Ignatus.
Washiriki wa Miss Arusha wapatao 22 wakiwa katika pozi ambapo tarehe 5julai mwaka huu atapatikana atakayekalia kiti cha miss Arusha 2019
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akiwasili katika hotel ya Kibo Palace tayari kwa uzinduzi wa mashindano ya kumsaka miss Arusha 2019.
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akisalimiana na mmoja wawalimbwende wanaoshindania taji la Miss Arusha 2019.
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akikata utepe ishara ya uzinduzi rasmi wa mashindano hayo ya miss Arusha 2019
Mgeni rasmi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC akizungumza katika uzinduzi rasmi wa misa Arusha 2019
Walimbwende wakiwa wanatembea mara baada ya kumpokea mgeni rasmi katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha
Walimbwende wakiwa wanatembea mara baada ya kumpokea mgeni rasmi katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPCakizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo
Walimbwende wanaoshindania taji la Miss Arusha wakiwa wanafungua Shampein mara baada ya mgeni rasmi kuzindua rasmk mashindano hayo.
Basil Elias meneja wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha , Tilly Chizenga mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019 wakigonganisha glass pamoja nalimbwende kama ishara ya uzinduzi wa mashindano hayo

Mgeni rasmi Msaidizi wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Basil Elias meneja wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha , Tilly Chizenga mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019 wakigonganisha glass pamoja nalimbwende kama ishara ya uzinduzi wa mashindano hayo.
Tilly Chizenga mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019.akizungumza na waandishi wa habari jatika uzinduzi wa Miss Arusha katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha leo.


Na.Vero Ignatus ,Arusha.


Mashindano ya miss Arusha yamezinduliwa rasmi leo jijini Arusha na Afisa Mnadhimu Mkoa (SO 1) ACP Kamishina msaidizi wa polisi katika hotel ya kibo palace iliyopo jijini hapa.

Tilly Chizenga ni mwekiti wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha2019 amesema uzinduzi huo unatoa fursa kwa warembo hao 22 kuingia kambini kuanzia kesho juni 8 hadi hapo yatakapo hitimishwa rasmi julai 5 mwaka huu. 

Arusha ametaja zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa amesema ni zawadi zenye mlengo na fursa kwa washindi ,ikiwemo nafasi ya masomo the east Africa institute na Mahusiano ya Kimataifa,fursa ya kimasomo kutoka TCI

Akizindua mashindano hayo Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi James Manyama msaidizi wa RPC Arusha amesema jeshi ka Polisi nchini wanaamini katika kutengeneza Raia wema waliolelewa katika ngazi ya familia Kidini mashuleni na vyuoni ambapo kazi ya jeshi hilo inakuwa rahisi zaidi kwani vibaka,majambazi hawana nafasi katika jamii.

Amesema Jeshi la polisi linaunga mkono mafunzo ya uraia mwema wanayopata walimbwende hao ambapo amewataka viongozi wakiona watahitaji mafunzo kutoka katika jeshi la polisi wapo tayari kwaajili yao.

"Sisi sote ni jamiii moja ya watanzania ambapo tukishirikiana kwa pamoja jamii zetu zitakuwa katika makuzi mema ambayo hayatakuwa na uhalifu.alisema"

Basil Elias meneja wa kamati ya maandalizi ya miss Arusha 2019 Kamati ya miss amesema kuwa kamati hadi warembo wenyewe wamejipanga kuhakikisha kwamba wanauwakilisha mkoa vizuri siyo kwenye ulimbwende tu bali hata katika utalii na jitihada hizo watazifanya hadi katika ngazi ya taifa .

Tumeshirikisha wadau mbalimbaki haswa warembo kuelezea namna mkoa wa Arusha uko juu katika maswala ya utalii.Amesema kuwa wamejioanga kutembelea maeneo mbalimbali katika wilaya ya Arusha mjini wilaya za jirani ili waweze kushirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali .

Tumeweza kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule namna ya matumizi sahihi taulo za kike ambapo ilienda sambaba na ugawaji wa taulo katika shule mbili Naurei na Sekei zote zikiwa za Arumeru.alisema

Amesema kuwa warembo hao hivi karibuni wameweza kushirikiana na jamii na wadau mbalimbali kutembelea kituo cha wazee cha mkoa wa Arusha kwaajili ya kutoa vyakula na huduma zingine.

This post appeared first on Mambo Pulse
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.