MCHOTEKA WAISHUKURU SERIKALI KWA UKARABATI WA KITUO CHA FYA [MamboPulse]
WANANCHI wa Kijiji cha Mchoteka kata ya Mchoteka wilayani Tunduru,wameishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Afya, jambo wanaloamini ukarabti huo utarahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu.
Aidha wamempongeza Rais Dkt John Magufuri kutokana na kazi nzuri anayofanyak kusimamia na kuboresha sekta ya Afya hapa nchini ambayo hapo nyuma ilikuwa na changamoto nyingi za kiutendaji ikiwemo uchakavu wa majengo na upungufu wa Dawa,vifaa tiba na watumishi katika hasa maeneo ya vijijini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana,baadhi ya wananchi Hussen Yusuf, Hausi Yasini na Ajika Kasembe wamesema, wana furahi sana kuona Serikali imeamua kutoa fedha ili kukarabati kituo cha Afya Mchoteka ambacho ni tegemeo kubwa kwa wananchi zaidi ya elfu nane na mia tano wa kata hiyo ambao kwa sasa wanalazimika kwenda hadi Hospitali ya MIsheni Mbesa kufuata huduma ikiwemo ya upasuaji.
Hussen alisema, hata hivyo bado litakuwa la upungufu wa Watumishi na kuikmba Serikali kuhakikisha mara ukarabati utakapokamilika ni vema kupeleka watumishi wa kutosha ambao watasaidiana na waliopo kuwahudumia wananchi.
Hamisi Yasini ameomba kazi ya ukarabati ikamilike haraka ili wananchi waweze kupata huduma ambazo zinakosekana katika kituo hicho kama upasuaji kwa wajawazito kwa kuwa hivi sasa wanalazimika kwenda vituo vingine hivyo kulazimika kutumia fedha nyingi na muda mwingi.
Alisema, ukarabati wa majengo hayo uendene na utoaji huduma bora kwa watu wakaofika kupata matibabu na kusisitiza kuwa,Serikali lazima iwachukulie hatua baadhi ya watumishi wenye lugha chafu kwa wagonjwa na wale wanaoendelea kufanya kazi kwa mazoea.
Naye fundi anayesimamia ujenzi huo Moshi Lukandamila alisema, hadi sasa ukarabati umefikia asilimia 85 na unatarajia kukamilika baada ya mwezi mmoja iwapo Serikali kupitia kamati ya ujenzi itapeleka vifaa kwa wakati.
Alisema, kwa sasa wanamalizia kuweka malumalu na kupaka rangi huku akitaja kuwa,kazi zote muhimu ikiwemo mfumo wa maji safi na taka, nyaya za umeme imeshakamilika.
Kwa upande wake,Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Dkt Wendy Robert alisema, ukarabti ulianza tangu Mwezi Agosti mwaka jana,lakini umechelewa kukamilika kutokana na upatikanji wa baadhi ya vifaa kama mawe ambayo yanapatikana mbali na eneo la ujenzi huo.
Kwa mujibu wa Dkt Wendy ukarabati wa kituo hicho kimsingi utasaidia sana wakazi zaidi ya 850 wa kata ya Mchoteka na wale wa kata jirani kama Nalasi kupata matibabu ya uhakika n ahata kukoa muda mwingi ambao walikuwa wanatumia kwenda maeneo mengine kufuata huduma.
Alisema, Serikali ya awamu ya tano imetoa shilingi Ml 400 kwa ajili ya ukarabati huo ukihusisha majengo matano ya upasuaji,mochwari,kichomeo taka, nyumba ya mtumishi na maabara ambayo yako katika hatua ya mwisho kukamilika.
Jengo la upasuaji linalojengwa katika kituo cha Afya Mchoteka wilayani Tunduru likiwa katika hatua ya mwisho kumalika ambapo litawezesha wananchi hasa akina mama wajawazito kupata huduma ya upasuaji.
Jengo la Wodi ya akina mama linalojengwa katika kituo cha Afya Mchoteka wilaya ya Tunduru ambalo limefikia asilimia 85 ya ujenzi wake,Serikali imetoa shilingi Milioni 400 ili kukarabati kituo hicho.
No comments