Neymar Awasilisha Taarifa kwa Polisi Kufuatia Madai ya Ubakaji [NimasikaForum]
Nyota wa Brazil Neymar alienda katika kituo cha polisi mjini Rio de Janeiro kuwasilisha taarifa kufuatia madai ya ubakaji , kulingana na wakili wake.
Nyota huyo amekana kumbaka Najila Trindade katika hoteli moja mjini Paris mnamo tarehe 15 mwezi Mei na kuwashukuru mashabiki wake nje ya kituo kwa usaidizi wao.
Bi Trindade aliwasilisha madai hayo Ijumaa iliopita akiambia runinga moja ya Brazil kwamba alikuwa anataka haki kutendeka.
Anasema kwamba wakati walipokutana na Neymar alikuwa mtu wa fujo ''mtu tofauti na yule niliyemjua katika ujumbe''.
Bi Trindade alikua amejiandaa kushiriki ngono lakini akataka watumie mipira ya kondomu. Anadai kwamba Neymar alikataa akaleta fujo na kumbaka.
Anasema kwamba alimwambia kuacha kufanya hivyo lakini akakataa.
Neymar aliwasili katika kituo cha polisi kwa kutumia magongo baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu wakati wa mechi ya Brazil dhidi ya Qatar mjini Brasilia siku ya Jumatano.
Wakili wake , Maira Fernandes aliambia Rueters : Neymar ametoa taarifa .
''Alichukua hatua ya kuja haraka ili kutoa taarifa , ili kuweka uwazi kila kitu kilichohitajika kuwekwa wazi''.
''Tuna matumaini kwamba tutahakikisha kua mteja wetu hana hatia. Mkakati ulikuwa mrefu lakini alitoa ufafanuzi uliohitajika''.
Akizungumza katika mlango wa kituo cha polisi, Neymar alisema: Nathamini usaidizi niliopata na ujumbe wote ambao ulimwengu umenitumia, marafiki zangu, mashabiki wangu, na ulimwengu uko nami. Nataka kusema ahsante sana kwa ujumbe huo wa kunipa moyo na nahisi kwamba ninapendwa sana''.

Kanda ya Video hapo juu inaonyesha mtafaruku kati ya bi Trindade katika chumba kimoja cha hoteli-ikidaiwa kuchukuliwa na bi Trindade.EXCLUSIVO! Assista ao vídeo da suposta briga entre Neymar e modelo que o acusou de agressão e estupro #JornalismoRecord #JornalismoVerdade pic.twitter.com/0K7N4mZe2X— Record TV (@recordtvoficial) June 6, 2019
Wawili hao wanaonekana wakiwa wamelala katika kitanda ambapo baadaye mwanamke huyo anasimama na kuanza kumpiga mwanamume aliyelala kitandani ambaye anajikinga na miguu yake.
Mwanamke huyo anasema nitakupiga, unajua kwa nini kwasababu umenipiga , mtafaruku huo ukionekana kuwa mkutano wao wa pili .
Neymar amesema kuwa yeye na bi Trindade walikutana mara mbili. Katika mahojiano hayo ya Runinga ya SBT , Bi Trindade alisema kuwa alianza kuelewa kila kitu kilichofanyika baada ya mkutano wao wa kwanza ulipokamilika na kwamba alirudi ili kuthibitisha kitendo kilichofanyika huku akitaka haki kufanyika.
Kanda hiyo ya Video ilionyeshwa katika kituo hicho cha Brazil.
No comments