tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

NIDHAMU YAWAONDOA MKUDE, AJIBU KIKOSI CHA TAIFA STARS YA AFCON 2019 [NimasikaForum]

Kocha Mkuu wa TaifaStars Emmanuel Amunike ametaja kikosi chake cha  wachezaji 32 wanaoondoka nchini leo kuelekea Misri kwaajili ya kambi ya wiki mbili kabla ya kutaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kitakachoshiriki AFCON2019 kuanzia Juni 21 mwaka huu.

Katika kikosi hicho Kocha Amunike amewaacha wachezaji saba kutoka kwenye orodha ya wachezaji 39 wa kikosi cha awali kilichotangazwa mapema mwezi Mei akitumia kigezo za nidhamu na kujituma kwao mazoezini.

Wachezaji walioachwa ni Ibrahim Ajibu (Yanga), Jonas Mkude (Simba SC), Ally Ally (KMC), Kennedy Juma (Singida United), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Khamis (Kagera Sugar) na Shomari Kapombe (Simba SC). Wachezaji 32 wanaoondoka leo ni:

Magolikipa
1. Aishi Manula - Simba SC.
2. Metacha Mnata - Mbao FC.
3. Suleiman Salula - Malindi FC.
4. Aron Kalambo - Tz Prisons.
5. Claryo Boniphace - U20.

Mabeki
6. Hassan Kessy - Nkana FC. 
7. Vicent Philipo - Mbao FC.
8. Gadiel Michael - Yanga SC.
9. Abdi Banda - Baroka FC
10. Ally Mtoni - Lipuli FC.
11. Mohamed Hussein - Simba SC.
12. Agrey Moris - Azam FC
13. Kelvin Yondan - Yanga
14. Erasto Nyoni - Simba SC.
15. David Mwantika - Azam FC.

Viungo wa kati
16. Feisal Salum - Yanga SC.
17. Himid Mao - Petrojet. 
18. Mudathir Yahya - Azam FC.
19. Frank Domayo – Azam FC
20. Fred Tangalu - Lipuli FC.

Viungo wa pembeni
21. Yahya Zayd - Ismailia.
22. Miraji Athuman – Lipuli FC.
23. Farid Musa – Tenerife.
24. Shiza Kichuya – ENPPI.
25. Saimon Msuva – Difaa El Jadidi.

Washambuliaji
26. Shaban Chilunda - Tenerife.
27. Rashid Mandawa – BDF.
28. Mbwana Samatta – KRC Genk.
29. Thomas Ulimwengu – JS Saoura.
30. John Bocco – Simba SC. 
31. Kelvin John – U17.
32. Adi Yusuph – Blackpool.

This post appeared first on Nimasika Forum
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.