tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

Rais wa FIFA Achaguliwa Bila Kupingwa [NimasikaForum]

Gianni Infantino amechaguliwa kuongoza shirikisho la soka duniani (FIFA), kwa muhula wa pili wa miaka minne, utakaokamilika mwaka 2023. 


Hatua hii imekuja baada ya kukosekana kwa mpinzani wa Infantino, wakati wa mkutano mkuu wa FIFA unaoendelea jijini Paris nchini Ufaransa. 


Infantino, mwenye umri wa miaka 49 raia wa Uswisi na Italia, alichaguliwa kuwa rais wa FIFA mwaka 2016 baada ya kuondoka kwa rais wa zamani Sepp Blatter. 


Baada ya kuchaguliwa tena, Infantino amesema kuwa, wakati wa miaka mitatu ambao amekuwa madarakani, taswira ya soka duniani imebadilika na kuwa na maendeleo makubwa.


This post appeared first on Nimasika Forum
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.