RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA TAASISI YA AL-HIKMA UKIONGOZWA NA SHEIKH NURDIN KISHKI IKULU ZANZIBAR [MamboPulse]
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation ya Jijini Dar es Salaam Sheikh Nurdin Muhammed Ahmed Kishki, alipofika IKulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 8-6-2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Al-Hikma Fundation ukiongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kulia Sheikh Nurdin Muhammed Ahmed Kishki, Sheikh Suleiman Khamis Habib,walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumsalimia leo 8-6-2019, (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Mwenyekiti wa Usalama na Itifaki na Mnadhimu Mkuu wa Al Hikma Fundation Sheikh Suleiman Khamis Habib, akitowa maelezo kuhusiana na Taasisi yao wakati wa mazungumzo hayo yaliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi,hayuko pichani baada ya kumaliza mazunguymzo na Ujumbe wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation ya Jijini Dar es Saalam ukiongonzwa na Mkurugenzi Mkuu Sheikh.Nurdin Muhammed Ahmed Kishki kulia Sheikh Suleiman Khamis Babib na Mussa Rajab Mushi, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Al – Hikma Foundation ya Jijini Dar es Salaam iikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo kulia Nurdin Muhammed Ahmed Kishki, Sheikh Suleiman Khamis Habib, Ndg. Mussa Rajab Mushi na Omar Hussein Mussa., Mwenyekiti wa Al -Hikma Foundation Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation Zanzibar, Sheikh Omar Hussein Mussa, akitowa neno la shukrani baada ya kumaliza mazungumzo hayo yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 8-6-2019, walipofika kumsalimia Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.,Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Taasisi ya Al -Hikma Foundation ya Jijini Dar es Salaam waliokaa kutoka kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Nurdin Kishki, Sheikh. Suleiman Khamis Habib na Sheikh.Omar Hussein Mussa na kulia Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Katibu Ofisi ya Mufti Mkuu Sheikh Fadhil Soraga na Mussa Rajab Mushi.(Picha na Ikulu)
No comments