SERIKALI YA DENMARK KUENDELEZA MSAADA PASS KWA AJILI YA WAKULIMA NCHINI.. [NimasikaForum]
Na Hussein Stambuli,Michuzi TV Morogoro.
Bolozi wa Denmark nchini Einar Jensen amesema kutokana na namna ambavyo Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo PASS inavyowawezesha vijana kwenye sekta ya kilimo wataendelea kutoa msaada kwa asasi hiyo kwani inamsaada mkubwa wa kuinua maisha ya vijana wajasiliamli wa kilimoTanzania ..
Balozi huyo alitembelea kituo atamizi cha SUA AIC na kujionea namna ambavyo Zaidi ya vijana 20 wanavyojifunza kwa vitendo ujasiliamali wa nyanya na ambapo alilidhidhwa na namna ambavyo PASS wameandaa utaratibu wa kilimo cha zao hilo kisasa.
“hiki wanachokifanya hapa vijana hawa ndicho kinachohitajika kwa kizazi cha sasa ninancho wasihi ni kuhakikisha mnazidi kuwa wavumbuzi na wabunifu Zaidi katika kila mnachokifanya nasisi tutakuwa bega kwa bega nanyi” alisema Balozi Einar
Mkurugenzi mkuu wa wa PASS Nicodemus Boay amesema vijana waliopo katika kituo hicho wanamoyo mkubwa wa kujikomboa kiuchumi kupitia ujasiliamli huo wa nyanya na anaamini kwa mafunzo na taaluma waliyopata wataweza kufika mbali kwani kupitia PASS watadhaminiwa kupata mikopo na kupata mitaji huku lengo likiwa ni vijana hao waweze kuajiri vijana wenzao.
“hawa vijana wakitoka hapa watachagua mahali pakwenda kufanyia shughuli zao na sisi kama PASS tutawashika mkono kuhakikisha wanafanikiwa kwa wanayotarajia kuyafanya katika mipango yao ya siku zijazo” alisema Boay
Meneja maendeleo biashara wa kituo hicho Richard Bruno ameeleza kuwa kuanzia mwezi Februari hadi Mei mwaka huu wameweza kujiingizia kiasi cha shilingi milioni 15 kupitia mradi wa kituo atamizi cha sua AIC hiyo ni kutokana na mavuno ya nyanya katika kipindi cha miezi mine.

Balozi wa Denmark nchini Einar Jensen akijadili jambo na kijana mjasiliamli wa zao la nyanya kuhusu uzalishaji wa zao hilo mkoani morogoro
Bolozi wa Denmark nchini Einar Jensen kushoto kwake mkurugenzi mkuu wa PASS nchini Nicodemus Boay akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa PASS pamoja na vijana wajasiliamali wa kituo atamizi cha SUA

No comments