Wakufunzi CCP wawazabua Wanafunzi CCP bonanza la Idd 2019 [NimasikaForum]
Timu ya Wakufunzi ya Chuo cha Polisi Tanzania imewazabua bila huruma timu ya wanafunzi ya chuo hicho kwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kusherehekea sikukuu ya Idd.
Mchezo huo ulicheza katika viwanja wa CCP Moshi mkoani Kilimanjaro ambako ilishuhudia ushindani mkali kwa timu zote mbili. Katika dakika 11 ya mchezo safu ya ulinzi ya Wakufunzi CCP iliharibu mipango ya safu ya ushambuliaji ya Wanafunzi kisha kuanza kwa haraka kwa pasi fupi hadi eneo la katikati ya uwanja.
Mpira ulipofika eneo hilo ulipigwa winga ya kushoto ambako nyota aliyeonekana kuisumbua sana safu ya ulinzi ya Wanafunzi Jeminus Hara alipoukimbiza mpira huo na kumlazimisha mlinzi wa kulia wa timu wa wanafunzi kumfuata.
Jeminus hakupoteza muda alipounasa mpira huo aliupiga kuelekea langoni mwa Wanafunzi CCP ambako Joshua Kamwela hakufanya makosa alipomalizia pasi hiyo iliyowashinda walinzi wa kati kisha kuipiga katikati ya miguu ya mlinda mlango wa Wanafunzi na kuandika bao katika dakika ya 12 ya mchezo.
Awali katika dakika ya pili ya mchezo Wanfunzi walianza kwa kasi walipovamia lango wa Wakufunzi na kushindwa kufunga kutokana na uimara wa mlinda mlango. Katika mchezo huo licha ya kuwa na kasi Wanafunzi walishindwa kutumia mianya waliyopata kupata walau bao la kufutia machozi.
Mwamuzi wa Ligi Kuu Sunday Komba alichezesha mchezo huo. Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa mkuu wa CCP Ramadhani Mungi ambaye alitoa mipira 15 na seti ya jezi kwa wachezaji wa timu mbili za U18 zilizoanza kwa kufungua bonanza hilo.
Mchezo wa fungua bonanza hilo baina ya watoto chini ya umri wa miaka zilizopewa majina katika bonanza hilo Coastal Union U18 na KMC U18 ulimalizika kwa sare ya bila kufungana. Michezo mingine kama kufukuza kuku, kuvuta kamba ilichezwa katika bonanza hilo. Kwa upande wa kufukuza kuku, Thomas Kiula na Mwita Chacha waliibuka washindi na kujinyakulia kuku waliowakamata.
Katika uvutaji wa kamba Maveterani wa Simba waliibuka washindi dhidi ya maveterani wa Yanga ambapo washindi walijichukulia kreti la soda.

![]() |
| Maveterani wa Yanga na Simba wakivuta kamba Juni 6, 2019 katika viwanja vya CCP Moshi kwenye bonanza la Idd. |
Awali katika dakika ya pili ya mchezo Wanfunzi walianza kwa kasi walipovamia lango wa Wakufunzi na kushindwa kufunga kutokana na uimara wa mlinda mlango. Katika mchezo huo licha ya kuwa na kasi Wanafunzi walishindwa kutumia mianya waliyopata kupata walau bao la kufutia machozi.
Mwamuzi wa Ligi Kuu Sunday Komba alichezesha mchezo huo. Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa mkuu wa CCP Ramadhani Mungi ambaye alitoa mipira 15 na seti ya jezi kwa wachezaji wa timu mbili za U18 zilizoanza kwa kufungua bonanza hilo.
Mchezo wa fungua bonanza hilo baina ya watoto chini ya umri wa miaka zilizopewa majina katika bonanza hilo Coastal Union U18 na KMC U18 ulimalizika kwa sare ya bila kufungana. Michezo mingine kama kufukuza kuku, kuvuta kamba ilichezwa katika bonanza hilo. Kwa upande wa kufukuza kuku, Thomas Kiula na Mwita Chacha waliibuka washindi na kujinyakulia kuku waliowakamata.
Katika uvutaji wa kamba Maveterani wa Simba waliibuka washindi dhidi ya maveterani wa Yanga ambapo washindi walijichukulia kreti la soda.
![]() |
| Mgeni rasmi wa Bonanza la Idd Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Ramadhani Mungi akiwakabidhi zawadi ya kreti la soda washindi wa Shindano la Kuvuta Kambi katika bonanza hilo. |
![]() |
| Mgeni rasmi Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Ramadhani Mungi akisalimiana na wachezaji wa Coastal Union U18 kabla ya kuanza kwa bonanza hilo dhidi ya KMC U18. |

No comments