tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

YANGA YAMUWANIA KWA HALI NA MALI NYOTA HUYU SIMBA [MamboPulse]


Imeelezwa kuwa mabosi wa klabu ya Yanga wako kwenye harakati nzito kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji wa Simba, Said Ndemla.

Ndemla ambaye anacheza nafasi ya kiungo, amekuwa hana msimu mzuri uliomalizika siku chache zilizopita kutokana na kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza.

Aidha, mchezaji huyo mkataba wake unaelekea ukingoni na hakuna dalili za mabosi wake kumuongezea mwingine.

Ni muda mrefu Yanga wamekuwa wakihusishwa na saini ya Ndemla ingawa wamekuwa wakifanya mambo yao kisirisiri.

Unaambiwa uongozi wa klabu hiyo unahaha kwa hali na mali ili kupata saini yake ukizingatia tayari timu yao imepata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.


This post appeared first on Mambo Pulse
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.