tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

DKT. MAGUFULI ASEMA YOTE YALIYOSEMWA NA WAFANYABIASHARA YATAFANYIWA KAZI [NimasikaForum]


Download


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini kuwa yote ambayo yamezungumzwa kwenye kikao kati yake na wafanyabishara hao yatafanyiwa kazi.

Akizungumza na wafanyabiashara hao leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo lengo la kikao hicho ilikuwa ni kujadili masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu changamoto za kwenye sekta ya biashara nchini.

Hata hivyo wakati anazungumzia baadhi ya changamoto na mapendekezo ya wafanyabishara hao, Rais Magufuli amefafanua yote yaliyojadiliwa na yanayoendelea kujadiliwa kati ya Serikali na wafanyabiashara yatapatiwa ufumbuzi na kufafanua kwa sasa Wizara ya Fedha na Mipango kuna mpango mkakati ambao wanauandaa na hivyo baadhi ya mambo yataingizwa.

"Wizara ya Fedha kuna mpango mkakati ambao wanaendelea kuuandaa na utakapokamilika utapelekwa Bungeni, hivyo niwahakikishie yote ambayo yamejadiliwa hapa tayataingizwa kwenye mpango huo kabla ya kwenda bungeni,"amesema Rais Magufuli.

Amefafanua kuna baadhi ya mambo ambayo yalizungumzwa mwaka jana kuhusu kupunguzwa kwa bei ya taulo za kike na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa tamko la Serikali ilitangaza kutoa punguzo lakini wafanyabishara hawajapunguza bei.

"Kuna wakati Serikali inakuwa na nia njema kwa kupunguza bei kwa baadhi ya bidhaa kwa mfano taulo za kike tuliamua kupunguza bei kutokana na maombi ya wananchi.Hata hivyo wafanyabishara wameshindwa kupunguza, hivyo lazima muwe na huruma,"amesema Rais Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka wafanyabiashara pamoja na Serikali kuweka mikakati ya kusonga mbele na kufafanua badala ya kuendelea kulalamika na kuendelea kulalamika kumesababisha Tanzania kuwa chini kwenye uuzaji wa biashara nje ya nchi.

Rais Dk. Magufuli amewataka wafanyabiashara kuaha woga na kueleza kuna vikwazo vingi ambavyo wanavipata kutoka Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini ukweli ni kwmaba kwenye kikao hicho wameshindwa kueleza kwasababu ya woga.

"Nilitarajia leo hapa wafanyabiashara mngewataja kwa majina watumishi wa TRA ambao wamekuwa wakiwasumbua lakini naona mmekaa kimya kwasababu mnaogopa.Acheni woga, ninyi wafanyabisara na Serikali tukiungana pamoja tutakwenda na tutapiga hatua,"amesema Rais Dk.Magufuli.

This post appeared first on Nimasika Forum
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.