tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

KUELEKEA MASHINDANO YA AFCON, VODACOM YAZINDUA KAMPENI YA DATA NA AFCON [NimasikaForum]

* Washindi kujipatia tiketi za kushuhudia na kushangilia timu ya taifa (Taifa stars) mubashara huko Misri

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania, leo Juni 7 imezindua rasmi kampeni mpya kwa wateja wao na mashabiki wa timu ya taifa inayoenda kwa jina la Data na AFCON ikiwa ni katika kutoa mchango wao wa kuishika mkono Taifa Stars inayoshiriki mashindano hayo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa idara ya biashara kutoka vodacom Linda Riwa amesema kuwa ndani ya kipindi cha kampeni hiyo watatoa zawadi kwa watumiaji kumi wa huduma ya soka letu ambao watajipatia tiketi za kuenda nchini Misri  kushuhudia na kushangilia timu ya taifa ikicheza mubashara kabisa.

Amesema kuwa kampeni hiyo imeanza rasmi leo na itamalizika Julai 21 na wateja watakuwa wakipata dondoo za mechi za ligi mbalimbali zinazoendelea duniani huku zawadi nyingine kemkemu zikiwemo muda wa maongezi na hiyo yote ni kwa kupiga *149*84# na kujiunga na huduma ya soka letu.

Bi. Riwa amesema kuwa kampeni hiyo imekuja kutokana na furaha baada ya timu ya taifa kufuzu kuwania kombe la AFCON hivyo wameona ni vyema kushirikiana na wateja wao ili kuweza kutia hamasa na morali zaidi kwa wachezaji na hatimaye kurudi na kombe hilo nyumbani.

Kwa upande wao wateja wa Vodacom; Juma Hamis wa Mbagala na Christian John wa Mwenge Dar es Salaam wameipongeza kampuni hiyo kwa kuonesha ushiriki wao katika masuala ya burudani hasa soka kwa kipindi hiki ambacho taifa limeelekeza macho yake nchini Misri kushuhudia michuano ya AFCON.
 Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Data na AFCON kupitia huduma ya soka letu iliyofanyika leo Juni 7, 2019 jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Meneja wa kitengo cha Vijana wa Vodacom, Abdi Zagar.




This post appeared first on Nimasika Forum
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.