ILALA YAKABILIANA NA DENGUE,KIPINDUPINDU KWA KUPULIZIA DAWA YA KUUA MBU ,VIMELEA VYA MAGONJWA..JANGWANI CHINI YA UANGALIZI WA MJEMA [MamboPulse]
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WILAYA ya Ilala jijini Dar es Salaam imeamua kupiga dawa ya kuua mazalia ya mbu wanaoneza homa ya dengue pamoja na kipindupindu katika eneo la Jangwani,Kariakoo na Mchikichini huku ikitangaza kuyaweka maeneo hayo chini ya uangalizi ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na wagonjwa ya mlipuko.
Wakati wa upuulizaji huo wa dawa ulioenda sambamba na usafi wa mazingira ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha wananchi kuendelea kusafisha mazingira ya maeneo yao,viongozi na watendaji wa Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wameshiriki upuliziaji dawa na kufanya usafi.
Akizungumza baada ya kupulizia dawa ya kuua mbu katika mtaro wa maji taka uliopo kwenye maeneo ya Jangwani,Mjema amesema maeneo hayo ndio yenye wagonjwa wengi wa kipundupindu na homa ya dungue.
Amesema hivyo Ilala wameweka mkakati wa kuhakikisha inapulizwa dawa maeneo yote ili wananchi wasiendelee kung'atwa na mbu wanaoneza Dengue.Pia ni mkakati wa Wilaya ya Ilala kukomesha kipindupindu ndani ya Wilaya hiyo na kwamba upuliziaji huo wa dawa u kwenda sambamba na usafi wa mazingira.
Mjema amesema eneo la kata ya Mchikichini na Kata ya Jangwani ndio kwa sehemu kubwa wananchi wake wamekupatikana na kipindupindu.",Hivyo mini pamoja na wenzangu wote tumekuwa maeneo haya kufanya usafi na kupuliza dawa kwenye maeneo yote tunayodhani yatakuwa na mazalia ya vimelea vinavyosababisha magonjwa ya mlipuko,"
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa maeneo ya Jangwani hali ni tete zaidi hasa kea kuzingatia maeneo hayo yalitawaliwa na mvua kasi cha wakati wa maeneo hayo kuyahama Makazi yao kwa muda,hivyo mkakati wa Wilaya ya Ilala ni kuendelea kuweka chini ya uangalizi.
Pia ameshauri kuwa kwa sasa wakazi wa Jangwani ni vema badala ya kukaa kwenye makazi hayo kuwa makini na ikiwezekana waaondoke hadi hali itakapokuwa salama kwa afya zao.Kwa upende wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Dk.Emily Lihawa amesema kutokana na kuwepo wa ugonjwa wa kipindupindu na Dengue wameona ni vema wakapiga dawa ya kuua mazalia ya mbu wa Dengue pamoja kipindupindu na kwa kuzingatia Kata ya Mchikichini,Jangwani na Kariakoo ndio zenye wagonjwa wengi hasa wa kipindupindu.
"Hatua ya kwanza ni hii ya kulipuza dawa kwenye mitarajo ya maji taka,na baada ya hapo tutapiga dawa kwenye makazi ya watu yakiwamo ya chooni. Eneo hili la Jangwani kuna watu wameupata kipindupindu na ndani ya Wilaya yetu kuna mwananchi mmoja amefariki kwa ugonjwa huo.Tumefanya pia usafi wa mazingira katika maeneo hayo,"amesema Dk.Lihawa.
Wakati huo huo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk.Tudas Ndungile amefafanua kuwa kuna mikakati mbalimbali imewekwa kukabiliana na homa ya dengue na kipindupindu,ukiwemo wa kuendelea kuhamasisha usafi wa mazingira na kupuuliza dawa ya kuua mazalia ya mbu na vimelea vya magonjwa hayo.
"Hivyo wakati sisi yuko hapa, maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaaam nako usafi unafanyika .Wilaya zote ziko kwenye usafi.Kama mnavyojua hadi sasa wakazi 98 wameugua kipindupindu,"amesema Dk.Ndungile.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema akishiriki kupuliza dawa ya kuua mbu na vimelea vya magonjwa ya homa ya dengue na kipindupi ndu katika eneo la Jangwani.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa amebeba vyombo cha kuhifadhia dawa ya kuua mbu wanaoneza homa ya dengue kabla ya kuanza kupuliza katika mtaro wa maji taka eneo la Jangwani
Mmoja watumishi wa Wilaya ya Ilala akiendelea kupuliza dawa ya kuua mbu wanaoneza homa ya dengue maeneo ya Kata ya Jangwani jijini Dar es Salaam
Upuliziaji dawa ya kuua mbu wanaoneza homa ya dengue pamoja na vimelea vya kipindupindu kuendelea eneo la Jangwani
Mmoja wa wapuliziaji dawa ya kuua mbu wa homa ya dengue akiwa ameweka began vyombo kilichohifadhiwa dawa kabla ya kuanza kupuliza katika eneo la Jangwani
Mtaro wa maji taka uliopo Kata ya Jangwani jijini Dar es Salaam ukiwa umezungukwa na makazi ya watu
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akizungumza na wananchi wa Jangwani baada ya kumalizika kwa upuliziaji dawa kwenye mtaro wa maji taka na makazi ya watu,ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na dengue pamoja na kipindupindu
No comments