tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU AHAMASISHA WANANCHI KUFANYA KAZI KWA BIDII,KUTUNZA VYANZO VYA MAJI [MamboPulse]

 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe tayari kabisa kwa kukimbizwa katika wilaya ya Arumeru, ambapo katika wilaya hiyo ina Halmashauri mbili, ambapo jumla ya miradi nane imezinduliwa Katika halmashauri ya Arusha na katika halmashauri ya Meru itakaguliwa na baadhi kuzinduliwa
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza jambo kabla ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe tayari kabisa kwa kukimbizwa katika wilaya ya Arumeru

 kiongozi wa mwenge wa uhuru  kiongozi wa Mbio za mwenge  wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ally akifungua shule ya sekondari ya odonyowas 

 Mazungumzo na Wafadhili
kiongozi wa Mbio za mwenge  wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ally akikata utepe ishara ya kuzindua mradi wa maji wa layout srwsita uliopo katika halmashauri ya Arusha Dc.


 Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mzee Mkongea Ally amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuendeleza kumpinga adui ujinga pamoja na kutunza vyanzo vya maji.

 Pia amesema Serikali  wameingia mikakati ya kuhakikisha  wananchi wanapata maji safi na salama kwa ajili ya wananchi wao huku akieleza kuwa Serikali imetenga kiasi cha  Sh.trilioni 9.2 kuhakikisha wananchi wao wanapata maendeleo.

Ally ameyasema hayo wakati akizindua miradi ,kuweka jiwe la msingi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo .Amesema   maji ni rasilimali nzuri inayochingia kuleta maendeleo ya nchi yetu, hivyo wananchi wanatakiwa kutunza mazingira hususa ni vyanzo hivi vya Maji. 

"Nakatika suala hili la kutunza vyanzo vya maji niwasihi  wananchi wenzangu kuacha kuchunga mifugo yetu katika vyanzo vya maji pamoja na nakuacha kufanya shughuli za kibinadamu  katika vyanzo vya maji, "Mzee Mkongea Ally.Pia amesema maji ni haki ya kila mtu, hivyo ni wajibu wa na kila mwananchi  kutunza vyanzo hivyo vya maji 

 Ameongeza kuwa hivi karibuni nchi inaelekea katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za vijiji pamoja na mitaa, hivyo amewataka wananchi hususa vijana na wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ambazo zinagombaniwa 

Pia amewataka wananchi kujitokeza kusikiliza sera za wagombea hao na kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi ambaye ataweza kuiongoza vyema na kuwaletea wananchi maendeleo

"Wananchi wenzangu jitokezeni kusikiliza sera za hawa viongozi wanaogombea ili muweze kufanya uchaguzi sahihi katika chaguzi za serikali zijaazo na msichague bora kiongozi bali chagueni kiongozi bora,"amesema.

Pia amewataka wananchi kulipa kodi kwani kodi ndio msingi wa kuleta maendeleo ya taifa letu, kwani kwakufanya hivyo ndiko kunatusaidia kuleta maendeleo katika halmashauri zetu na hata vijiji vyetu  
 
Katika mbio hizo za mwenge katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC imezindua miradi mbalimbali ikiwemo kuzindua na kufungua shule Ya sekondari ya Odonyowas, mradi wa maji wa layout Srwsita,mradi wa Nyuki pamoja na hospital ya mama na mtoto ya orturmenti.


This post appeared first on Mambo Pulse
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.