tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

SHERIA MPYA,HUWEZI TENA KUKOPEA KIWANJA,SHAMBA AMBALO HALIJAENDELEZWA HATA KAMA UNA HATIMILIKI. [NimasikaForum]

Na Bashir Yakub
Wiki iliyopita niliandika kuwa ujenzi wa fensi pekee kwenye kiwanja sio maendelezo halisi kwa mujibu wa kanuni mpya za sheria ya ardhi tofauti na tulivyozoea. Leo tena tunatizama Sehemu ya (iii) kanuni ya 7 ya kanuni mpya kanuni za Sheria ya Ardhi kupitia tangazo la serikali  namba 345 la tarehe 26/ 4 / 2019.
Kanuni ya 7(1) inasema kuwa mwenye kiwanja/shamba ambalo halijaendelezwa au lenye maendelezo hafifu,endapo ataomba mkopo na kuweka rehani ardhi hiyo, atatakiwa ndani ya miezi sita tokea siku alipoweka rehani, apeleke taarifa kwa kamishna wa ardhi kuonesha ni  namna gani pesa yote au sehemu ya pesa alizokopa zimetumika katika kuendeleza ardhi husika.
Kutokana na kanuni hii maana yake ni kuwa ardhi unayokopea inatakiwa kuwa imeendelezwa au kama haijaendelezwa basi kiasi cha pesa unachopata kupitia mkopo lazima kitumike kuendeleza ardhi hiyo uliyotumia kukopea bila kujali umekopa hela ili kuzifanyia nini. Na hii ni kwa ardhi zenye hatimiliki. Mwenye ardhi atatakiwa ndani ya miezi sita  tokea kuweka ardhi yake rehani apeleke taarifa maalum kwa kamishna wa ardhi kuonesha ni namna gani hela yote au sehemu ya hela aliyoipata ilivyotumika kuendeleza ardhi aliyoweka rehani.
MFANO, una kiwanja chenye hatimiliki, lakini hakijaendelezwa(un-developed) au kimeendelezwa lakini maendelezo hafifu(under-development) kama kujenga fensi tu, au kijumba kibovu cha mlinzi nk.Sasa unaomba mkopo benki wa Tsh milioni 50 na rehani yako ni kiwanja hicho. Benki wao watatizama na kuona kuwa kiwanja unachoweka rehani hakijaendelezwa au kina maendelezo hafifu.

                                       KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com


This post appeared first on Nimasika Forum
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.