TCRA YAENDELEA KUJIKITA KUTOA ELIMU ZAIDI YA USAJILI WA LAINI KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE [NimasikaForum]
Wakazi wa Dodoma na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Mkuu wa TCRA Kanda ya Kati Mhandisi Antonio Manyanda amesema ni fursa kwa wananchi wa Dodoma kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano.
Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano.
Manyanda amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
"TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Manyanda.
Wananchi wakikamilisha usajili wa Laini za Simu kwa Kutumia alama za vidole. Katika Mnada jijini Dodoma.
Wananchi wakiwa katika Mnada na kupata huduma za mawasiliano katika Mnada huo jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Bidhaa za Mawasiliano Thadayo Ringo akitoa maelekezo kwa Wananchi wa Dodoma katika kampeni ya Mnada kwa Mnada inayoendeshwa na TCRA
Mwananchi wa Dodoma akiweka alama za vidole kwa ajili ya laini za simu.
Timu ya TCRA ikiwa katika picha ya pamoja katika kampeni ya Mnada kwa Mnada jijini Dodoma.









No comments