tanzaniapulse link

Header pulse

 MTAFUTE HAPA NDUGU AU JAMAA MLIOPOTEZANA?

"TANZIA TANZIA MSIBA LUTON - UINGEREZA [MamboPulse]



*Ndugu Wanafamilia na Watanzania Wote Waishio UK *

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza TZUK DIASPORA kwa masikitiko makubwa inawatangazia taarifa ya msiba wa Mke wa mwanajumuiya mwenzetu Abdulkadir Rashid , Bi Rachel Maona kilichotokea  leo asubuhi tarehe 08/06/2019 Keech Hospices - Luton nchini Uingereza.

Marehemu Bi. Rachel Maona ambaye alikuwa akifanya kazi Luton and Dunstable Hospital nchini Uingereza alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kansa na ameacha watoto watatu na mume. 

Taratibu za msiba na kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinaendelea kufanywa kwa kushirikiana na East Africa Muslim Community na Luton Tanzanian Community , Kwa kushirikiana na watanzania wanaoishi UK.

Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki  Uongozi kwa niaba ya familia ya tunawaomba ushirikiano wenu na faraja kwa familia.


UONGOZI 

JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO UK (TZUK DIASPORA

This post appeared first on Mambo Pulse
 Download
 Play

No comments

Powered by Blogger.