TANZIA *TANZIA * MSIBA LUTON,UINGEREZA-TANZANIA [MamboPulse]
*Ndugu Wanafamilia na Watanzania Wote Waishio UK *
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza TZUK DIASPORA kwa masikitiko makubwa inawatangazia taarifa ya msiba wa Mke wa mwanajumuiya mwenzetu Abdulkadir Rashid , Bi Rachel Maona kilichotokea leo asubuhi tarehe 08/06/2019 Keech Hospices - Luton nchini Uingereza.
Marehemu Bi. Rachel Maona ambaye alikuwa akifanya kazi Luton and Dunstable Hospital nchini Uingereza alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kansa na ameacha watoto watatu na mume.
Taratibu za msiba na kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinaendelea kufanywa kwa kushirikiana na East Africa Muslim Community na Luton Tanzanian Community , Kwa kushirikiana na watanzania wanaoishi UK.
Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki Uongozi kwa niaba ya familia ya tunawaomba ushirikiano wenu na faraja kwa familia.
UONGOZI
JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO UK (TZUK DIASPORA
No comments